• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Wakulima wa Korosho mtwara wana deni la shirili bilioni 1.4

    (GMT+08:00) 2019-08-07 19:13:43

    Benki ya Wananchi Zanzibar (PBZ) tawi la Mkoa wa Mtwara, inadai Jumla ya Sh. bilioni 1.4 ikiwa mikopo iliyobaki mikononi mwa wakulima, waliyokopeshwa mwaka wa fedha 2018/2019.

    Hayo yameelezwa na Ofisa Masoko wa Benki hiyo, Nassir Mohamed Zaid, alipokuwa akizungumza kwenyeMaonyesho ya Wiki ya Wakulima Nanenane katika viwanja vya Ngongo, Manispaa ya Lindi.

    Zaid alisema kiasi hicho kinachodai ni miongoni mwa mikopo ya Sh. bilioni 2.8 iliyotolewa kwa wanachama wakulima zaidi ya 2,000, vikiwamo vyama vya msingi na ushirika (AMCOS) 50 katika mikoa ya Mtwara na Lindi mwaka 2018/2019.

    Alitaja maeneo ya wakulima walionufaika na mikopo hiyo ni wa Tandahimba, Newala, Namnyamba, Masasi mkoani Mtwara pamoja na kata mbili za Mkoa wa Lindi, ikiwamo ya Mnolela.

    Zaid alisema katika mikopo iliyotolewa mwaka huo, kiasi kilichorejeshwa kwenye benki hiyo ni Sh. bilioni 1.4 sawa na asilimia 50 ya fedha zilizotolewa kwa mikopo msimu uliopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako