• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia: AfDB yaidhinisha ruzuku ya dola milioni 98 kwa Ethiopia

    (GMT+08:00) 2019-08-07 19:14:32

    Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imeidhinisha ruzuku ya dola milioni 98 za ujenzi wa barabara itakayounganisha Ethiopia na Djibouti.

    Gharama ya jumla ya mradi huo ni dola milioni 255 milioni, na inajumuisha ruzuku ya AfDB ya milioni 98 kwa serikali ya Ethiopia na ruzuku ya AfDB ya dola milioni 5.3 kwa serikali ya Djibouti, pamoja na mchango wa fedha wa dola milioni 151 na serikali ya Ethiopia.

    Taarifa kutoka kwa AfDB inasema mradi huo utaimarisha biashara kwa kupunguza gharama za usafirishaji, na hivyo kuharakisha ukuaji wa uchumi wa Ethiopia na Djibouti, kwani ni sehemu ya barabara kuu ya usafirishaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako