• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Tanzania kunufaika na maonesho ya viwanda

  (GMT+08:00) 2019-08-07 19:17:44

  Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, amesema Wiki ya Maonyesho ya nne ya viwanda ya nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ni fursa pekee ya kutangaza bidhaa zinazozalishwa nchini humo

  Alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukagua mabanda kwenye maonyesho hayo yanayoendelea kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.

  Maonyesho hayo ambayo yalifunguliwa juzi na Rais John Magufuli, yanafanyika katika maeneo matatu ambayo ni JNICC, viwanja wa Gymkhana na viwanja vya Karimjee.

  Waziri Mkuu alisema fursa hiyo ni muhimu kwa Watanzania kuonyesha bidhaa za ndani ili wageni wanaokuja wajue kuna bidhaa zipi zinazozalishwa nchini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako