• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KUOGELEA: Ssengonzi kuogelea kwenye mashindano ya All Africa Games Morocco

    (GMT+08:00) 2019-08-08 08:59:49

    Muogeleaji kutoka Uganda anayeishi Marekani Rebecca Ssengonzi amerejea kwenye timu ya taifa akiwa tayari kwa michuano ya All Africa Games itakayoanza Agosti 19 na kumalizika Agosti 28 huko Rabat, Morocco. Awali Ssengonzi hakupatikana kwenye michuano ya mabingwa wa dunia iliyomalizika hivi karibuni nchini Korea Kusini lakini sasa anaweza kujiunga na timu ya waogeleaji wa Uganda wakiwa wanafukuzia nafasi kwenye mashindano ya olimpiki mwakani. Bahati nzuri kwa upande wake safari za Afrika kaskazini zimekuwa zikizaa matunda. Mwaka jana alifanikiwa kushinda medali ya shaba alipoogelea kwa mita 50 kwenye Michuano ya Vijana ya Afrika. Mwaka 2015 pia alishinda medali ya fedha na shaba kwenye michuano ya Africa Junior Swimming Championships huko Cairo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako