• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema pande mbalimbali za Syria zinatakiwa kumaliza tofauti ili kupata suluhisho la kisiasa

    (GMT+08:00) 2019-08-08 09:12:05

    Naibu balozi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao amesema, pande zinazopigana nchini Syria zinatakiwa kumaliza tofauti kwa njia ya majadiliano na kutafuta suluhisho la kisiasa kwa pamoja.

    Bw. Wu amesema hayo katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja huo kuhusu wafungwa, mateka na watu wasiojulikana walipo uliofanyika jana, na kuongeza kuwa pande mbalimbali za Syria zinatakiwa kufanya juhudi kwa kuzingatia siku za baadaye za nchi hiyo na maslahi ya msingi ya wananchi. Pia amesema pande hizo zinatakiwa kumaliza tofauti kwa njia ya mazungumzo, kuhimiza makubaliano ya amani na kutafuta utatuzi wa kisiasa unaofuata hali halisi ya nchi hiyo.

    Akizungumzia msimamo wa China kuhusu suala hilo, Bw. Wu amesema kuwa China ina wasiwasi kuhusu hali ya kibinadamu na maisha ya watu wa Syria. Amesema jumuiya ya kimataifa inatakiwa kuendelea kutoa misaada ya fedha na vitu kwa watu wa nchi hiyo na kuunga mkono juhudu za serikali na watu wa Syria za kujenga upya nchi yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako