• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SGR yaingiza faida,asema waziri wa uchukuzi Kenya,Dkt James Macharia

  (GMT+08:00) 2019-08-08 19:24:49

  Waziri wa Uchukuzi,Barabara na Ujenzi nchini Kenya,Dkt James Macharia,amesema reli ya kisasa (SGR) imeingiza faida ya Sh400 milioni.

  Akizungumza mjini Murangá jana,Dkt Macharia alisema SGR inaingiza biashara ya Sh2.2 bilioni huku gharama zikiwa ni Sh1.82 bilioni hivyo basi kushikilia kuwa hiyo ni hesabu ya faida.

  Aidha reli ya SGR inaingiza faida tele katika uchukuzi wa abiria na faida hiyo inatarajiwa kuongezeka wakati biashara ya uchukuzi wa mizigo itakaposhika kasi.

  Wakati huohuo Dkt Macharia alipuuza madai kuwa kwa sasa SGR ni mradi wa hasara.

  Dkt Macharia alifafanua kwamba ukadiriaji katika kipindi cha mwaka wa kifedha wa 2019/20, ni kuwa pato kwa mwezi kutoka huduma za SGR litakuwa Sh3.3 bilioni.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako