• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yailalamikia Marekani baada ya ofisa wake kuwasiliana na kiongozi wa kundi linalotetea Hong Kong kujitenga

  (GMT+08:00) 2019-08-08 20:19:12

  Msimamizi husika wa Ofisi ya Kamishna wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China katika Hong Kong leo amemwita ofisa mwandamizi wa konseli kuu ya Marekani katika Hong Kong na Macao, akitoa malalamiko makali na kutaka upande wa Marekani ueleze wazi kufuatia ripoti kuwa ofisa wa konseli hiyo alikutana na kiongozi wa kundi la watu wa Hong Kong wanaotetea eneo hilo kujitenga na China.

  Msimamizi huyo amesisitiza kuwa China ina nia thabiti katika kulinda usalama wa mamlaka ya taifa na ustawi na utulivu wa Hong Kong, na inapinga nchi yoyote, kundi lolote na mtu yoyote kuingilia kwa njia yoyote mambo ya Hong Kong. Amewataka wafanyakazi wa konseli kuu ya Marekani Hong Kong wafuate sheria ya kimataifa na kanuni za kimsingi za uhusiano wa kimataifa, kukumbuka wajibu wao, kujitenga mara moja na watu wanaoipinga China na kuvuruga hali ya Hong Kong, kusimamisha mara moja kutoa ishara zisizo sahihi kwa wahalifu na wale wanaotumia mabavu, kutoingilia mambo ya Hong Kong na kurekebisha makosa yao haraka.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako