• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Biashara kati ya China na nchi za nje yakua kwa haraka licha ya changamoto zilizopo

  (GMT+08:00) 2019-08-08 20:19:45

  Biashara kati ya China na nchi za nje imeendelea kuwa na ongezeko kubwa katika miezi saba ya mwaka huu, licha ya changamoto za ndani na nje.

  Idara kuu ya forodha ya China imesema biashara ya bidhaa imeongezeka kwa asilimia 4.2 na thamani yake kufikia dola trillion 2.49 kuanzia mwezi January hadi Julai.

  Bidhaa zinazouzwa nje zimeongezeka kwa asilimia 6.7 kwa kipindi hicho na thamani yake imefikia dola trillion 1.34, na bidhaa zinazoagizwa kutoka nje zimeongezeka kwa asilimia 1.3 na thamani yake imefikia dola trilioni 1.12. Faida iliyopata China imeongezeka kwa asilimia 47.4 na kufikia dola milioni 212.

  Idara hiyo pia imesema katika kipindi hicho Umoja wa Ulaya umeendelea kuwa mshirika mkubwa wa biashara wa China, ukifuatiwa na nchi za ASEAN na Marekani. Biashara kati ya China na nchi za "ukanda mmoja, njia moja" iliongezeka kwa asilimia 10.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako