• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA-Timu ya Tanzanite yatinga fainali kombe la COSAFA baada ya kuibanjua Afrika Kusini

    (GMT+08:00) 2019-08-09 09:42:33

    Timu ya taifa ya wanawake chini ya umri wa miaka 20, Tanzanite imefanikiwa kutinga Fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Kusini mwa Afrika (COSAFA) baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Afrika Kusini jana jioni Uwanja wa Gelvandale mjini Port Elizabeth. Mabao ya Tanzanite yamefungwa na Enekia Kasonga dakika ya 18 na Opa Clement Sanga dakika ya 30. Baada ya mchezo huo, mchezaji wa Tanzanite, Enekia Kasongo alichaguliwa Mchezaji Bora wa Mechi, timu hiyo ikiendelea kutoa mchezaji wa mechi zote ilizocheza. Sasa Tanzanite itakutana na Zambia katika fainali Jumapili, ambayo imeitoa Zimbabwe kwa kuichapa 1-0, bao pekee la Mary Mambwe dakika ya 32. Huo utakuwa mchezo wa pili kuzikutanisha timu hizo, baada ya Zambia kuichapa Tanzania 2-1 kwenye mchezo wa mwisho wa Kundi B.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako