• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Gazeti la The Wall Street Journal la Marekani laonya sera isiyo sahihi ya kibiashara itasababisha kushuka kwa uchumi wa nchi hiyo

  (GMT+08:00) 2019-08-09 17:25:06

  Gazeti la The Wall Street Journal la Marekani limetoa tahariri inayoonya juu ya sera isiyo sahihi ya kibiashara iliyotolewa na serikali ya rais Donald Trump wa Marekani, na kusema itasababisha kushuka kwa uchumi wa nchi hiyo.

  Makala hiyo imemkosoa moja kwa moja mshauri wa kamati ya biashara ya ikulu ya Marekani Bw. Peter Navarro baada ya habari kusema kuwa, washauri wote wa kiuchumi wa rais Donald Trump walikataa kuongeza ushuru mpya dhidi ya China isipokuwa Bw. Navarro.

  Makala hiyo pia imesema, tangu mgogoro wa kibiashara utokee mwaka 2018, imani na uwekezaji wa makampuni ya Marekani vimeendelea kupungua na kuanza kuathiri vibaya ongezeko la uchumi wa nchi hiyo. Pia imesema, China haikudhibiti kiwango cha ubadilishaji wa sarafu, na kwamba mabadiliko ya thamani ya sarafu yake yanatokana na uhusiano wa utoaji na mahitaji.

  Wakati huohuo, wachambuzi wa uchumi wa China wanaona kuwa, kitendo cha wizara ya fedha ya Marekani cha kuiorodhesha China kama nchi inayodhibiti kiwango cha ubadilishaji wa fedha, si tu kimekwenda kinyume cha vigezo vilivyowekwa na nchi hiyo, bali pia kimeonesha jinsi serikali ya Marekani inavyocheza mchezo wa kutumia vigezo viwili kukandamiza mshindani wake, na kwamba ilifumba macho wakati serikali hiyo ilipoishinikiza Benki Kuu kupunguza viwango vya riba.

  Kwa muda mrefu, baadhi ya wamarekani wamedai China iongeze unyumbufu wa kiwango cha ubadilishaji wa sarafu yake RMB, lakini hivi sasa, wakati kiwango hicho kinabadilika, wao wanailaumu China kuwa inadhibiti kiwango cha safaru, kauli zao zinakinzana sana.

  Wakati huohuo, Benki Kuu ya Marekani tarehe 31, Julai ililazimika kutangaza kupunguza viwango vya riba wakati hali ya uchumi a haijafikia masharti yanayoruhusu hatua hiyo. Wenyeviti wanne wa zamani wa Benki hiyo wametoa makala kwa pamoja kwenye gazeti la The Street Journal wakipinga kitendo hicho na kusema, Marekani inahitaji Benki Kuu iliyo huru. Pia wametoa wito kuhakikisha uamuzi wa sera ya fedha ya Marekani hauathiriwi na shinikizo la siasa la muda.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako