• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tasaf yawezesha ujenzi barabara na kilimo cha miti

  (GMT+08:00) 2019-08-09 18:39:37

  Wananchi wa Kijiji cha Murgina Kata ya Mabawe na Kijiji cha Munyenzi wilayani Ngara mkoani Kagera nchini Tanzania wametumia nguvu kazi kutengeneza barabara yenye urefu wa kilomita 8.5 na kuwekeza kilimo cha miti ekari 14 ili kurahisisha uhamishaji wa mazao pamoja na uhifadhi mazingira.

  Miradi hiyo imeweza kuwapatia ujira wanufaika na mpango wa kunusuru kaya maskini Tasaf kama sehemu ya kuwapatia kipato chenye kuboresha maisha yao kwani miradi hiyo iko chini ya serikali ya kijiji kwa manufaa ya wananchi wakiwamo walengwa wa mpango huo.

  Utekelezaji wa mpango wa Tasaf 3 sehemu ya kwanza ulidumu kwa muda wa miaka mitatu na sehemu ya pili ya mpango huo utaanza Agosti mwaka huu.

  Serikali ya Tanzania ilileta wazo la kuanzisha kutengeneza barabara ya vumbi baada ya kuona wakulima wanahangaika kutoa mazao shambani.

  Aidha, mradi huo ulipoanzishwa vijana wenye uwezo wa kufanya kazi walipatiwa ajira ya kulipwa kwa eneo shilingi elfu 5,000 ikiwa nyenzo zilizotumika ni majembe na koleo.

  Naye Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora), Dk. Mery Mwanjelwa, alisema ubunifu wa miradi hiyo ya kudumu unufaishe walengwa wote na kuhakikisha wanaweza kusimama wenyewe kwa maisha yao.

  Alisema wataalamu ambao wameingia na kusaidia elimu ya utarayarishaji mashamba ya miti na kuboresha barabara watumike pia kuwapatia sehemu sahihi ya soko.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako