• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wakulima wa EAC watakiwa kuboresha bidhaa zao kuvutia nje

  (GMT+08:00) 2019-08-09 18:41:30

  Wakulima wa kanda ya Afrika mashariki wametakiwa kuhakikisha kuwa bidhaa zao zinahifadhiwa na kushughulikiwa ipasavyo ili kuvutia soko la nje.Wakizungumza kwenye mkutano wa siku tatu mjini Kampala Uganda, wajumbe kutoka Umoja wa Ulaya, Kituo cha biashara ya kimataifa na wajumbe wa jumuia ya Afrika mashariki, wamesema mafanikio ya kanda hii yanategemea mtandao mzuri wa kilimo biashara. Wamesema ijapokuwa bidhaa za kanda hii kama vile kahawa na chai zimewavutia wengi katika soko la kimataifa wakulima wa kanda hii wanatakiwa kuboresha zaidi bidhaa hizo. Mwanauchumi wa Afrika mashariki Bw Charles Omusala amesema kilimo kinashikilia asilimia 30 za pato la taifa katika kanda hii na kutoa ajira kwa karibu asilimia 90 ya watu katika kanda ya Afrika mashariki.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako