• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yasema uingiliaji wowote wa mambo ya Hong Kong utapingwa vikali

  (GMT+08:00) 2019-08-09 18:59:35

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema uingiliaji wa mara kwa mara wa Marekani kwenye maswala ya Hong Kong utakutana na upinzani mkali kutoka kwa watu wote wa China ikiwa ni pamoja na wale wa Hong Kong.

  Bibi Hua amesema hayo baada ya msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani kusema kuwa kitendo cha kutaja taarifa binafsi za ofisa wa konseli yake ya Hong Kong aliyewasiliana na wafarakanishaji wa Hong Kong hakikubaliki, na kwamba mkutano kati ya wanadiplomasia wa Marekani na wapinzani wa serikali za nchi nyingine ni wa kawaida.

  Bibi Hua amesema msemaji huyo anatakiwa kutafakari kwanza maneno yake kabla ya kuanza kuikosoa na kuichafua serikali ya China, na ameongeza kuwa kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine ni tabia ya kawaida ya wanadiplomasia wa Marekani, lakini Hong Kong ni ya China na wachina hawatakubali kutukanwa au kuburuzwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako