• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kampuni ya Huawei yazindua mfumo wake wa uendeshaji wa vifaa vya kielekroniki

  (GMT+08:00) 2019-08-09 19:00:04

  Kampuni ya Huawei imezindua mfumo wake wa uendeshaji wa vifaa vya kielekroniki (OS).

  Akiongea mjini Dongguan, mkoani Guangdong, mkuu wa kampuni ya Huawei Bw. Richard Yu amesema kabla ya kutambulisha mfumo huo, kampuni yake ilifikiria mahitaji ya baadaye ya wateja, kwamba watahitaji mfumo unaoweza kutumika kwenye vifaa vyote.

  Amesema mfumo huo hauna utata na una usalama wa hali ya juu, na umelenga muunganiko wa vifaa mbalimbali vya mtandao wa internet, lakini kwanza utatumia kwenye vifaa vinavyovaliwa, skrini za kisasa, mifumo ya magari na spika za kisasa.

  Pia amesema licha ya changamoto zinazoikumba kampuni hiyo kutokana na vikwazo vilivyowekwa na serikali ya Marekani, kampuni ya Huawei imeweza kupata ongezeko la asilimia 24 kutokana na mauzo yake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako