Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limefanya mkutano wa dharura kuhusu hali ya Libya na kulaani vikali shambulizi la bomu lililotegwa ndani ya gari katika mji wa Benghazi mashariki ya nchi hiyo, na kusisitiza kuwa Umoja wa Mataifa hautaondoka katika nchi hiyo.
Wafanyakazi watatu wa Tume Maalumu ya Umoja wa Mataifa nchini Libya wameuawa kwenye shambulizi hilo, na wengine wengi wakiwemo wafanyakazi watatu wa Umoja wa Mataifa kujeruhiwa.
Mwenyekiti wa zamu ya mwezi huu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambaye pia ni mwakilishi wa kudumu wa Poland katika Umoja huo Bi. Joanna Wronecka, ametoa salamu za rambirambi kwa jamaa za wahanga wa tukio hilo..
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |