• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watu 28 wafariki dunia baada ya kimbunga cha Lekima kuikumba sehemu ya mashariki mwa China

  (GMT+08:00) 2019-08-11 17:49:29

  Watu 28 wamefariki na wengine 20 hawajulikani walipo baada ya kimbunga cha Lekima kuukumba mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China.

  Sehemu kubwa ya vifo hivyo vimetokea katika kaunti ya Yongjia, mjini Wenzhou ambako mvua kubwa zinazonyesha zimesababisha maporomoko ya udogo yaliyozuia mito. Kingo za ziwa zimepasuka na mafuriko kusomba watu.

  Ofisi ya mkoa ya kupambana na mafuriko imesema watu karibu milioni 1.08 wamehamishwa katika sehemu salama, na karibu watu milioni 5 wameathiriwa.

  Ofisi hiyo pia imesema katika mkoa wa Zhejiang kimbunga hicho kimeharibu hekta zaidi ya laki 1.73 za mashamba na kuharibu nyumba elfu 34, na thamani ya hasara za moja kwa moja za kiuchumi imefikia dola za kimarekani bilioni 2.1.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako