• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yaitaka Uingereza isiingilie kati mambo ya Hong Kong

  (GMT+08:00) 2019-08-11 17:51:11

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying, amesema mambo ya Hong Kong hayatakiwi kuingiliwa na nchi yoyote ya kigeni, na China inaitaka Uingereza isimamishe mara moja kuingilia kati mambo ya Hong Kong, na mambo ya ndani ya China.

  Bibi Hua Chunying amesema Hong Kong ya leo ni eneo lenye utawala maalum la China, na siyo koloni la Uingereza. Uingereza haina mamlaka, madaraka ya utawala, na madaraka ya usimamizi katika Hong Kong.

  Kwa mujibu wa sheria ya kimsingi ya Hong Kong, mambo ya nje ya eneo hilo yanashughulikiwa na serikali kuu ya China. Kitendo cha serikali ya Uingereza kumpigia simu moja kwa moja na kumshinikiza ofisa mkuu wa eneo la utawala maalum la Hong Kong si sahihi.

  Bibi Hua amesema hayo kufuatia habari kutoka kwa msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Uingereza, kuwa waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo amempigia simu Bibi Carrie Lam kuhusu hali ya Hong Kong.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako