• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzanite yalipa kisasi, ikibeba ndoo ya Cosafa

  (GMT+08:00) 2019-08-12 09:15:58

  Timu ya Taifa ya Tanzania kwa wanawake chini ya miaka 20 Tanzanite jana mchana imefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya Soka ya Nchi za Ukanda wa Kusini mwa Afrika (COSAFA Women) kwa kuifunga Zambia mabao 2 – 1. Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Wolfson, mjini Port Elizabeth nchini Afrika Kusini, Tanzanite ilipata bao lake la kwanza kupitia kwa Opa Sanga katika dakika ya 24 na bao la pili lililofungwa na Protasia Mbunda katika dakika ya 84. Goli hilo liliwafanya wachezaji wa Zambia waishiwe na nguvu kutokana na kusalia dakika 6 kabla ya mechi hiyo kumalizika.
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako