• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yatekeleza sera inayotoa kipaumbele katika utoaji wa nafasi za ajira

  (GMT+08:00) 2019-08-12 17:44:57

  Takwimu kuhusu nusu ya kwanza ya mwaka huu zilizotolewa na Wizara ya raslimali watu na huduma za jamii ya China zimeonesha kuwa, ongezeko la watu wanaopata ajira mijini na vijijini limefikia milioni 7.37, ambacho ni asilimia 67 ya lengo lililowekwa kwa mwaka mzima. Mkutano wa baraza la serikali la China umesema, katika kipindi kijacho China itachukua hatua zenye nguvu zaidi kutuliza ukuaji wa uchumi, kusaidia ujasiriamali na kuongeza utoaji wa nafasi za ajira.

  Hizi ni siku ambazo wanafunzi waliohitimu Vyuo Vikuu wanaanza kutafuta ajira. Mkurugenzi wa Kituo cha utoaji wa huduma kwa watu wenye elimu ya juu wanaotafuta ajira kilichoko mkoani Anhui Bw. Wu Chuan anasema:

  "Kila mwanafunzi aliyehitimu kutoka chuo kikuu anatakiwa kupewa zaidi ya mara tatu huduma zinazohusika. "

  Mkuu wa Idara ya kuhimiza upatikanaji wa nafasi za ajira iliyo chini ya Wizara ya rasilimali watu na huduma za jamii ya China Bibi Zhang Ying ameeleza kuwa, mwaka 2019 kuna jumla ya wanafunzi milioni 8.34 waliohitimu vyuo vikuu, hivi sasa utaratibu wa utoaji wa nafasi za ajira unaendelea kwa utulivu, na kiwango cha upatikanaji wa ajira kimeongezeka zaidi ya miaka kadhaa iliyopita. Katika kpindi kijacho, wizara hiyo itachukua hatua mbalimbali kusaidia wanafunzi waliohitimu vyuo vikuu mbalimbali wanapata ajira.

  Mkutano wa Ofisi ya kisiasa ya Kamati Kuu ya chama cha Kikomunisti cha China umesisitiza tena kuwa, maendeleo ya uchumi wa China yanakabiliana na matishio mapya. China inapaswa kushughulikia vizuri mambo yake yenyewe, kutuliza utoaji wa nafasi za ajira, mambo ya fedha, biashara ya nje, fedha za kigeni, uwekezaji, na makadirio ya ukuaji wa uchumi. Ikiwa ni kipaumbele cha maisha ya wananchi, utoaji wa nafasi za ajira umewekwa katika nafasi ya kwanza katika kazi mbalimbali za serikali. Mtafiti wa Baraza la serikali la China Bw. Yao Jingyuan anasema:

  "Watu watapata fedha baada ya kupewa ajira, na maisha yao yataweza kuboreshwa. Ndio maana utoaji wa nafasi za ajira ni muhimu sana kwa maisha ya wananchi."

  Bw. Yao pia anaona kuwa, katika nusu ya pili ya mwaka huu, China inapaswa kufuata msingi wa kupata maendeleo ya uchumi kwa hatua madhubuti, na kuendelea na sera chanya ya kuhimiza utoaji wa nafasi za ajira, ili kuboresha hali ya upatikanaji wa ajira kwa kuchukua hatua mbalimbali kutoa nafasi nyingi zaidi za ajira.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako