• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yalaani vikali vitendo vya mabavu dhidi ya polisi wa Hong Kong

    (GMT+08:00) 2019-08-12 20:05:56

    Msemaji wa ofisi ya mambo ya Hong Kong na Macau ya baraza la serikali la China Bw. Yang Guang hapa Beijing amelaani vikali wahuni waliofanya uhalifu mkubwa dhidi ya polisi wa Hong Kong.

    Amesema, jana usiku baadhi ya wahuni walitupa mabomu ya mafuta kwenye vituo vya polisi huko Tsim Sha Tsui, Cheung Sha Wan na makao makuu ya polisi huko Wan Chai, na kusababisha askari polisi kujeruhiwa, na pia amewapa pole askari polisi waliojeruhiwa.

    Wakati huohuo, mkuu wa ofisi ya serikali kuu ya China huko Hong Kong pia ametoa taarifa akilaani vikali vitendo vya mabavu vyenye msimamo mkali vilivyofanywa na wahalifu wachache, huku akihimiza jamii nzima kuchukua hatua kuunga mkono kithabiti serikali ya Hong Kong na polisi kuzuia vurugu, kurejesha utaratibu na kulinda kwa pamoja utawala wa kisheria na usalama wa jamii wa Hong Kong.

    Habari nyingine zinasema, kuanzia Agosti 8 hadi 12 polisi wa Hong Kong wamewakamata watu 149 wanaotuhumiwa kufanya maandamano haramu, kuwashambulia polisi, kuzuia utekelezaji wa sheria na kukamatwa na silaha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako