• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwendesha mashtaka mkuu wa Washington nchini Marekani apinga sera mpya ya wahamiaji

    (GMT+08:00) 2019-08-13 09:55:21

    Mwendesha mashtaka mkuu wa jimbo la Washington nchini Marekani Bw. Bob Ferguson ameweka wazi msimamo wake wa kupinga sera "dhidi ya wahamiaji" itakayotangazwa na serikali ya nchi hiyo ndani ya siku mbili zijazo.

    Serikali ya Marekani inapanga kutangaza rasmi marekebisho ya sera ya "malipo ya umma", ambayo yatawafanya wahamiaji wenye kipato cha chini wakabiliwe na changamoto zaidi katika kupata haki ya kudumu ya kuishi nchini Marekani au kadi ya kijani.

    Bw. Ferguson amesema, sera hiyo mpya itawaruhusu maofisa wa uhamiaji kuwachukua wahamiaji wanaotumia moja ya huduma za jamii zikiwemo ruzuku za makazi, afya na chakula kama mzigo wa jamii wakati wowote katika siku za baadaye, na kukana hadhi yao halali mpya au iliyopo sasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako