• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisa mkuu wa Hongkong atoa wito wa kusimamisha matukio ya kimabavu na kurejesha utaratibu wa kawaida

    (GMT+08:00) 2019-08-13 17:13:32

    Ofisa mkuu wa Mkoa wa Utawala Maalumu wa Hong Kong Bibi Carrie Lam Cheng Yuet-ngor leo amesema, watu walioandamana mkoani Hongkong wiki iliyopita, walipuuza sheria na kushambulia maofisa wa usalama wakiwemo polisi, ili kutimiza lengo la kuharibu utawala wa sheria. Amesema utawala wa sheria ni kiini muhimu kwa Hongkong, lakini hivi sasa jamii ya mkoa huo imeingia kwenye mvutano mkubwa, , na itahitaji muda mrefu kurejea hali ya kawaida.

    Bi. Carrie Lam Cheng Yuet-ngor ameeleza wasiwasi wake mkubwa kutokana na hali iliyotokea mkoani Hongkong wiki iliyopita. Matukio makubwa ya uharibifu yakiwemo kufunga njia ya reli chini ya bahari na ile juu ya ardhi, hali iliyoathiri vibaya wakazi wanaoenda kazini, pia tarehe 12, Uwanja wa Kimataifa wa Hongkong uliathiriwa vibaya na waandamanaji jambo lililolazimu ni kusitisha kazi. Waandamanaji walishambulia vituo vya polisi, na kuwashambulia maafisa wa polisi kwa silaha na kuwatupia mabomu ya petroli. Anasema:

    "Tumeshuhudia matukio mengi ya kukiuka sheria kwa kisingizio cha uhuru au haki, ambayo yameharibu utawala wa Hongkong, na kututia wasiwasi mkubwa. Utawala wa sheria ni kiini cha Hongkong, ikiwa utavurugwa, vitu vingine vingi pia vitavurugika."

    Ofisa huyo pia amesema, ili kutimiza lengo la kuvunja utawala wa sheria, baadhi ya watu walishambulia taasisi za usalama ikiwemo kikosi cha polisi, kuchochea chuki dhidi ya polisi na kuwamwagia matope.

    "Kikosi chenye idadi ya polisi elfu 30 ni nguzo muhimu ya utawala wa sheria ya Hongkong. Matukio yaliyotokea wiki iliyopita yanatia wasiwasi mkubwa kwamba, Hongkong inayochukuliwa kama ni jamii yenye kuheshimu utawala wa sheria, itakabiliwa na hatari kubwa, na itachukua muda mrefu kwa kurejea hali ya kawaida."

    Bi. Carrie Lam Cheng Yuet-ngor amesisitiza kuwa, kipaumbele kwa sasa ni kupambana na vitendo vya kimabavu, kulinda utawala wa sheria, na kurejesha utaratibu wa jamii. Amewataka wahongkong kuacha maoni tofauti na kutulia, na kuanzisha ujenzi wa jamii yenye masikilizano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako