• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uvutiaji wa fedha za kigeni wa China katika miezi saba iliyopita mwaka huu waongezeka

  (GMT+08:00) 2019-08-13 19:10:53
  Takwimu zilizotolewa na Wizara ya biashara ya China zimeonyesha kuwa kuanzia mwezi Januari hadi mwezi Julai, China imetumia fedha za kigeni Yuani bilioni 533.14, ikiwa ni ongezeko la asilimia 7.3 kwa kulinganishwa na mwaka uliopita wakati kama huu, na ongezeko la mwezi Julai limekuwa asilimia 8.7 likilinganishwa na mwezi Julai mwaka uliopita.

  Naibu mkurugenzi wa idara ya fedha za kigeni ya Wizara ya biashara ya China Bw. Zhu Bing amesema kuwa miezi saba iliyopita matumizi ya fedha za kigeni yameongezeka kwa utulivu, na sekta za utengenezaji na utoaji wa huduma za teknolojia ya hali ya juu zimeongeza kwa kasi.

  Bw. Zhu ameongeza kuwa kutokana na hamu kubwa ya kuvutia uwekezaji nchini China, uwekezaji wa fedha za kigeni wa Umoja wa Ulaya umeongeza na kuwa asilimia 18.3 , na uwekezaji wa Ujerumani nchini China umeongeza na kuwa asilimia 72.4, aidha ongezeko la uwekezaji wa Korea Kusini na Japani nchini China limekuwa asilimia 69.7 na asilimia 72.4.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako