• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kituo maalum chatakiwa kwa kukusanya asali

  (GMT+08:00) 2019-08-13 19:14:22
  Serikali nchini Tanzania imeombwa kuwatafutia wavuna asali kituo maalumu cha ukusanyaji zao hilo kutoka mashambani ili iwe rahisi kuwabaini baadhi ya watu wanaochakachua asali kabla haijaingia sokoni.

  Wadau kwenye sekta hiyo wanasema ni muhimu serikali kuwa na kituo maalumu cha kukusanyia asali zao kwa ajili ya kuiuza kwa wafanyabiashara ili kuondokana na tabia ya baadhi wanaochakachua bidhaa hiyo.

  Wanasema hivi sasa ni vigumu kupata asali inayofanana kwa sababu kila mmoja anakusanya asali kivyake na kuileta sokoni jambo ambalo sio rahisi kuwabaini wanaochakachua.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako