• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • CAF yasogeza mbele mechi ya Simba, JKT Tanzania

  (GMT+08:00) 2019-08-14 08:51:54
  Mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Simba na JKT Tanzania, iliyokuwa imepangwa kuchezwa Agosti 23, imesogezwa mbele hadi Agosti 29, mwaka huu, kutokana na mwingiliano ya michuano ya Kimataifa. Kwa mujibu wa ratiba ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Simba watakuwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, kucheza na UD Songo ya Msumbuji katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika. Kocha wa timu ya JKT Tanzania, Abdallah Mohammed 'Bares', amesema wamepata barua kuwa mechi yao na Simba itachezwa Agosti 29, hivyo hakuna kitakachoharibika. Bares alisema kutokana na mabadiliko ya ratiba hiyo wataendelea kutumia muda uliopo kufanya maandalizi wakiwa kambini Zanzibar, ikiwamo kucheza mechi nyingi za kirafiki.
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako