• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya yapoteza mechi ya pili magongo ya kutafuta tiketi Olimpiki 2020

  (GMT+08:00) 2019-08-14 09:15:11

  Matumaini ya timu ya wanaume ya Kenya kurejea katika Olimpiki katika fani ya mpira wa magongo mwaka 2020 yamedidimizwa zaidi baada ya kupoteza mechi ya pili kwenye mchujo wa Afrika kwa kucharzwa 7-2 na Misri katika mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Chuo Kiku cha Stellenbosch nchini Afrika Kusini, hapo jana. Kenya ilifungwa mabao matatu ya haraka, na kujikuta ikiwa imefungwa mabao 4-0 wakati wa mapumziko. Kenya ilijikakamua katika kipindi cha pili na kupunguza mwanya huo kupitia kwa Constant Wakhura dakika ya 33 baada ya kupata kona fupi. Kabla hata ya kusheherekea bao hilo, Misri iliongeza mabao mengine mawili na hivyo kudidimiza ndoto za timu hiyo ya Kenya kufuzu fainali za mpira wa magongo kwa mwaka 2020. Kichapo hiki ni cha pili mfululizo kwa Kenya iliyotupa uongozi mara mbili ikipepetwa 3-2 na Ghana katika mechi yake ya ufunguzi mnamo Agosti 12.

  Kwa upande wa timu ya wanawake ya mgongo ya Kenya, timu hiyo imepata alama moja muhimu dhidi ya Ghana japo kwa jasho katika mechi yake ya pili ya kina dada kwenye mchujo wa mpira wa magongo wa Afrika wa kufuzu kushiriki Olimpiki mwaka 2020, ambayo ilimalizika kwa sare ya 1-1 nchini Afrika Kusini katika mechi iliyochezwa jana. Rhoda Kuira aliifungia Kenya bao la mapema katika dakika ya saba kutokana na kona fupi. Hata hivyo, kutoka hapo warembo hao walishambuliwa hadi kipenga cha mwisho. Mashambulizi makali ya Ghana yalishuhudia ikisawazisha 1-1 kupitia kwa Mavis Berko kutokana na kona fupi. Wakenya waliponea mara kadhaa kuadhibiwa na Ghana kwa kupoteza mipira kwa urahisi. Matokeo haya yaliendeleza rekodi nzuri ya Kenya kutoshindwa na Ghana katika mechi za kufuzu kushiriki Olimpiki hadi mechi nne.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako