• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchumi wa China kwa mwezi wa Julai waendelea kukua kwa utulivu

    (GMT+08:00) 2019-08-14 17:12:35

    Takwimu zilizotolewa leo na Idara Kuu ya Takwimu ya China zinaonesha kuwa, mwezi Julai uchumi wa China umeendelea kukua kwa kasi inayofaa. Katika kipindi kijacho, China itaimarisha uhamasishaji wa uvumbuzi kwa uchumi, na kuongeza uhai wa soko, ili kuhimiza uchumi wa China kuendelea vizuri kwa utulivu na mfululizo.

    Takwimu zilizotolewa na Idara Kuu ya Takwimu ya China zinaonesha kuwa, mwezi Julai thamani ya uzalishaji wa viwanda nchini CHina iliongezeka kwa asilimia 4.8 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huo. Msemaji wa idara hiyo Bi. Liu Aihua anasema,

    "Uwekezaji wa sekta ya viwanda umeongezeka kwa asilimia 3.3, na kasi ya ongezeko la uwekezaji huo imefufuka kidogo kwa miezi mitatu mfululizo. Wakati huohuo, uwekezaji kwa sekta za uhifadhi wa mazingira na elimu umeongezeka kwa asilimia 41 na 18.5."

    Takwimu hizo pia zinaonesha kuwa sekta ya huduma hususan huduma za kisasa imekua kwa kasi, na katika miezi 7 iliyopita ya mwaka huu, alama ya uzalishaij wa huduma nchini China imeongezeka kwa asilimia 7.1. Kwa upande wa ajira, katika miezi hiyo, China imeongeza ajira milioni 8.67, na kumaliza asilimia 80 ya mpango wa mwaka huu.

    Hata hivyo, baadhi ya alama za uchumi zimeshuka katika mwezi Julai. Bi. Liu amesema hii ni hali ya kawaida, na kwa jumla uchumi wa China umedumisha ongezeko la kasi inayofaa, akisema,

    "Kufuatia mwelekeo wa alama za maendeleo ya uchumi, zikiwemo kasi ya ongezeko la uchumi, ajira na bei ya bidhaa, tunaweza kuona kuwa hivi sasa uchumi wa China unaongezeka kwa kasi inayofaa. Kwani kiwango cha sekta za uchumi kinainuka kwa mfululizo, mahitaji ya ndani yanaboreshwa na kuongezeka, uwekezaji wa nje na biashara kati ya China na nchi za nje inaongezeka, na bei ya bidhaa imedumisha utulivu."

    Bi. Liu amesema hivi sasa China inazingatia zaidi kuongeza uhai wa soko, kuimarisha nguvu ya ndani ya uchumi, kuboresha mazingira ya biashara, na kupunguza kodi na ada. Amesisitiza kuwa China ina imani, uwezo na msingi wa kudumisha maendeleo mazuri ya uchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako