• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Idadi ya watumiaji wa mtandao wa Internet wa China yafikia milioni 830 hadi mwishoni mwa mwaka 2018

  (GMT+08:00) 2019-08-14 18:58:06

  Ripoti iliyotolewa na idara ya takwimu ya taifa ya China imesema, idadi ya watumiaji wa mtandao wa Internet wa China imeongezeka kutoka laki 6.2 ya mwaka 1997 hadi milioni 830 ya mwaka 2018. Mwaka 2018 matumizi ya mtandao wa simu za mkononi yalifikia GB bilioni 71.1, ambayo ni mara 56.1 ya mwaka 2013.

  Ripoti hiyo imeonesha kuwa teknolojia ya habari na mawasiliano TEHAMA imetimiza maendeleo makubwa. Hadi mwishoni mwa mwaka jana, idadi ya watumiaji wa mtandao wa mkonga wa mawasiliano imefikia milioni 368 na idadi ya watumiaji wa mtandao wa 4G imefikia bilioni 1.17. Idadi ya watumiaji wa simu kote nchini China imefikia bilioni 1.75 ambayo inashika nafasi ya kwanza duniani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako