• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pigo KMC: Mugiraneza, Bokungu kuwakosa AS Kigali

    (GMT+08:00) 2019-08-15 08:35:31
    Baadhi ya nyota wa kigeni wa klabu ya KMC wataikosa mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya AS Kigali ya Rwanda itakayochezwa Agosti 23. Sababu za nyota hao kukosa mechi hiyo ni kuchelewa kupatikana kwa leseni zao kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na pia kuchelewa kwa hati zao za uhamisho wa kimataifa (ITC). Meneja wa KMC Faraji Muya amesema uwezekano wa nyota hao kucheza mechi ya marudiano ni mdogo sana kwa kuwa hawataweza kupata nyaraka hizo kwa wakati. Wakati huohuo, klabu hiyo imeanza mazoezi rasmi ya kujiandaa na mikwaju ya penalti kuelekea mchezo wao wa marudio dhidi ya AS Kigali utakaochezwa mwishoni mwa wiki ijayo. Katika mechi yao ya kwanza iliyochezwa Rwanda, timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana, hivyo mchezo wa marudiano unatakiwa kupata matokeo tofauti ili moja kati ya timu hizo iweze kusonga mbele na mashindano hayo.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako