• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bei ya mafuta yashuka Zanzibar

    (GMT+08:00) 2019-08-15 18:24:47
    Mamlaka ya udhibiti wa huduma za maji na nishati Zanzibar (ZURA) imetangaza bei mpya ya mafuta ambayo iliamza kutumika jana.

    Akitangaza bei hizo jana katika ofisi za mamlaka hiyo ,Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano,Khuzaimat Bakari Kheri,sababu ya kushuka kwa bei za mafuta ni kutokana na kushuka kwa bidhaa hizo katika soko la kimataifa.

    Bei ya mafuta ya petroli kwa mwezi huu Zanzibar ni Sh2,181 kutoka Sh2,338 mwezi uliopita.

    Mafuta ya dizeli yameshuka kwa asilimia 4.23 na sasa yanauzwa Sh2,221 kutoka Sh2,319.

    Mkuu huyo wa mawasiliano alisema mafuta ya taa yatauzwa Sh1,675 kwa lita kutoka Sh1,753 mwezi uliopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako