• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mamlaka ya uwanja wa ndege wa Hong Kong yasema uwanja huo umerejea kufanya kazi

    (GMT+08:00) 2019-08-15 20:06:23

    Mamlaka ya uwanja wa ndege wa Hong Kong imesema shughuli za kuruka na kutua kwa ndege zimeanza tena na maegesho ya garinamba moja na nne yamefunguliwa kwa umma.

    Ofisi hiyo imesema kuwa jana uwanja huo umeshughulikia ndege 1000, na hivi sasa agizo la kuzuia kwa muda lililotolewa na mahakama linaendelea kufanya kazi na kuzuia mtu yeyote kuzuia kazi za uwanja wa ndege kwa njia haramu na makusudi, na abiria wenye tiketi au kitambulisho wanaruhusiwa kuingia kwenye jengo la uwanja wa ndege.

    Mamlaka hiyo imesisitiza kuwa kuhakikisha kazi za uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hong Kong, na usalama wa abiria na wafanyakazi ni kipaumbele cha jukumu lake, na kulaani tukio la kimabavu lililotokea kwenye uwanja huo na kutoa salamu za pole kwa majeruhi wa tukio hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako