• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio ya kimabavu yatakapokuzuiliwa ndipo mazingira ya biashara ya Hongkong yataokolewa

  (GMT+08:00) 2019-08-15 20:38:26

  Matukio ya kimabavu yanayozidi kupamba moto mitaani yanaidhuru vibaya Hongkong, na kuitumbukiza Hongkong kwenye shimo la mgogoro uliozushwa na watu. Hongkong ikiwa moja kati ya makundi ya kiuchumi yenye nguvu kubwa ya ushindani duniani inaingizwa kwenye shimo la hatari, na mazingira yake mazuri ya biashara yanayosifiwa na watu yanaharibiwa vibaya kwa makusudi mabaya.

  Mazingira mazuri ya biashara yana umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya Hongkong, lakini matukio yanayoendelea ya kimabavu yanaua mazingira ya biashara, kuharibu imani ya jumuiya ya kimataifa kwa Hongkong, na endapo hayatazuiliwa yataathari vibaya maendeleo ya Hongkong.

  Kipaumbele cha Hongkong ni kuzuia vitendo hivyo vya kimabavu, na kamwe haitawezekana kuufanya mkoa huo wenye uhai mkubwa kuvunjika kwa nguvu za kimabavu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako