• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Macho kwa Chager madereva 23 wakiwania taji la Kilifi Rally

  (GMT+08:00) 2019-08-16 08:05:40
  Dereva Baldev Chager atalenga kuendeleza ubabe wake Mbio za Magari za Kitaifa za Kenya (KNRC) zinapoingia duru ya nne hii leo. Ingawa dereva Onkar Rai ameorodheshwa kuondoka jukwaani wa kwanza katika duru hii ya KCB Kilifi Rally, Chager, ambaye alinyakua mataji ya duru mbili zilizopita za KCB Kajiado Rally na Safari Rally, ndiye anapigiwa upatu mkubwa kutifulia wenzake vumbi. Chager, ambaye kwa kawaida huendesha gari la aina ya Mitsubishi Evolution 10, alikuwa amejawa na tabasamu katika mahojiano kabla ya Kilifi Rally. Alisema anaingia duru ya Kilifi akiwaheshimu wapinzani wake, licha ya kuwa alibeba mataji ya duru mbili zilizopita. Anasema yeye na mwelekezi wake Ravi Soni watajitahidi kadri ya uwezo wao kufanya vyema. Hata hivyo, Chager, ambaye ana nafasi kubwa ya kuongeza mwanya wa alama kati yake na mpinzani wake wa karibu Carl Tundo, alikiri kuwa magari ya Skoda Fabia R5s yatatoa ushindani mkali sana.
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako