• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kufufuka kwa uchumi wa Hong Kong kunahitaji kumalizika kwa vurugu

    (GMT+08:00) 2019-08-16 08:58:49

    Ofisa Mkuu wa Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong China Bi. Carrie Lam amesema, mkoa huo unakabiliwa na hali tete ya kiuchumi, na ufufukaji wake unahitaji kumalizika kwa vurugu na kurejeshwa kwa utawala wa sheria.

    Katika ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Facebook, Lam amesema hali ya sasa ya uchumi wa Hong Kong ni mbaya sana, na inahusiana kwa karibu na kila mtu katika mkoa hyo.

    Awali, katibu wa Fedha wa serikali ya mkoa huo Paul Chan alitangaza hatua kadhaa za kuunga mkono kampuni na kulinda ajira. Lam amesema, hatua hizo zinalenga kusaidia kampuni ndogo na za ukubwa wa kati kukabiliana na hali inayodorora ya kiuchumi na kupunguza mzigo kwa watu.

    Habari nyingine zinasema, kamishina wa Ofisi ya wizara ya mambo ya nje ya China katika mkoa wa Hong Kong Bw. Xie Feng amesema vurugu zinazoendelea Hong Kong hazihusiani na masuala ya haki za binadamu wala uhuru na demokrasia, bali ni jaribio linalofanywa na wapinzani na watu wenye itikadi kali la kupindua serikali halali ya mkoa wa Hongkong kwa njia haramu na za kimabavu.

    Msemaji wa ofisi hiyo amesisitiza kuwa serikali na watu wa China wana dhamira thabiti ya kulinda mamlaka, usalama na maslahi ya taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako