• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sheria kuhusu viazi kuunganisha wadau

    (GMT+08:00) 2019-08-16 18:59:32
    Wadau katika sekta ya kilimo cha viazi nchini Kenya sasa watalazimika kuingia katika miungano wanapofanya shughuli zao.

    Kulingana na sheria mpya zinazolinda kilimo cha viazi, inataka kubuniwe vituo maalumu ambako wakulima wa viazi watakuwa wakipeleka mazao yao kwa wanunuzi, hivyo basi kuwatoa nje madalali ambao wamekuwa wakiingia mashambani kununua viazi hivyo.

    Lengo la sheria hizo mpya ni kutoa mwongozo na kuimairhsa mapato katika kilimo cha viazi, kupanua mawazo ya jinsi ambavyo kinaweza kutumika kuendelea maisha mema ya mkulima na wale washika dau wote wanaounganishwa na kilimo hicho.

    Wiki hii, afisa mkuu wa kilimo serikalini Bw Joel Kibet amesema wakulima hivi sasa ni lazima watiii sheria hizo mpya.

    Sheria hizo mpya vile vile zinazitaka serikali za kaunti kuhakikisha kwamba viazi ambavyo vinauziwa wananchi ni bora kiafya na ni vya thamani ambayo inaweza kufaidi mkulima pamoja na wahusika wengine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako