• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watu wa hali mbalimbali wa Hongkong wapinga vitendo vya kimabavu

  (GMT+08:00) 2019-08-17 18:21:53

  Watu wa hali mbalimbali wa mkoa wa utawala maalumu wa China Hongkong wameeleza kuunga mkono serikali na polisi ya mkoa huo kuzuia vurugu, na kulinda ustawi na utulivu wa mkoa huo.

  Shirikisho la utamaduni wa China la Hongkong limesema, vurugu zilizotokea mkoani humo zimekuwa na dalili ya ugaidi, na zimeleta matishio makubwa kwa utawala wa kisheria na utulivu wa jamii.

  Shirikisho la kuhimiza utamaduni katika vyuo vikuu la Hongkong limeunga mkono polisi kulinda usalama wa jamii na maisha ya watu.

  Mwenyekiti wa bodi ya Kampuni ya Henglong Bw. Chen Qirong amesema, kila mkazi wa Hongkong mwenye roho safi anapaswa kupinga vitendo vya kimabavu, na kuiunga mkono serikali kurejesha utaratibu wa jamii.

  Naye msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bi Hua Chunying amesema, hivi sasa kazi muhimu zaidi ni kumaliza vurugu na kurejesha utaratibu wa jamii mkoani Hongkong.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako