• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mjumbe wa China kwenye Umoja wa Mataifa atoa wito wa kutumika njia ya amani kutatua suala la Kashmir

  (GMT+08:00) 2019-08-17 18:22:20

  Mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Zhang Jun, amesema Suala la Kashmir linapaswa kutatuliwa kwa njia ya amani kulingana na mkataba wa Umoja wa Mataifa, azimio husika la Baraza la Usalama na makubaliano ya pande mbili.

  Akiongea na wanahabari baada ya mashauriano ya baraza la usalama, Bw. Zhang amesema suala la Kashmir ni suala linalotokana na historia kati ya India na Pakistan. Amebainisha kuwa kulingana na azimio husika hali ya Kashmir haijaamuliwa na ni eneo lenye machafuko linalotambulika kimataifa.

  Baraza la Usalama jana lilifanya mashauriano yasiyo rasmi juu ya suala la India na Pakistan na kusikiliza taarifa zilizotolewa na sekretarieti ya Umoja wa Mataifa juu ya hali ya Jammu na Kashmir na Kazi ya kundi la Waangalizi wa Kijeshi la Umoja wa Mataifa huko India na Pakistan. Wajumbe wa baraza wamesema wana wasiwasi mkubwa juu ya hali ya sasa na kutarajia kuwa pande husika zitajizuia na kutochukua hatua za upande mmoja ambazo zitaongeza hali ya mvutano.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako