• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yapinga vikali mpango wa Marekani wa kuiuzia silaha Taiwan

  (GMT+08:00) 2019-08-17 19:12:31

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying tjana alisema kuwa, China inapinga vikali mpango wa serikali ya Marekani wa kuiuzia Taiwan ndege za kivita za F-16V , nakutoa malalamiko yake kwa Marekani.

  Bibi Hua alisema kuwa, kitendo hiki cha Marekani kimekiuka kanuni ya kuwepo kwa China moja tu na taarifa tatu za pamoja za China na Marekani, hasa taarifa ya "8.17", na kuingilia kati mambo ya ndani ya China pamoja na kudhuru mamlaka na maslahi ya usalama wa China.

  Bibi Hua alisisitiza kuwa suala la Taiwan linahusiana na mamlaka na ukamilifu wa ardhi na maslahi makuu ya China. China inaitaka Marekani kutambua madhara ya suala hilo na kuacha kuiuzia silaha Taiwan na kusitisha mawasiliano ya kijeshi kati yake na Taiwan.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako