• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu wa hali mbalimbali waendelea kulaani vurugu Hong Kong, China

    (GMT+08:00) 2019-08-18 17:24:26

    Watu wa hali mbalimbali na sehemu mbalimbali duniani wameendelea kulaani vurugu na vitendo vya kimabavu vilivyotokea katika mkoa wa utawala maalumu wa China Hong Kong.

    Gazeti la Wen Wei la Hong Kong limetoa tahariri likisema, ongezeko la vitendo vya kimabavu litadhuru watu wote wa Hong Kong, na jamii zote zinapaswa kushikamana na kuzuia wahalifu wasiendelee kuvuruga Hong Kong.

    Umoja wa Kulinda Hong Kong jana alasiri uliitisha mkutano wa hadhara, na kutaka maandamano haramu na vitendo vya kimabavu vikomeshwe, na watu wenye maoni tofauti ya kisiasa wavumiliane badala ya kushambuliana.

    Wizara ya mambo ya nje ya Russia imesema madhumuni ya nchi za magharibi kuingilia mambo ya Hong Kong ni kuharibu utulivu wa China.

    Habari nyingine zinasema, serikali ya Hong Kong imesema mtu yeyote haruhusiwi kuvichukulia vyuo vikuu kama sehemu za kudai maslahi ya kisiasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako