• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la TMC la Sudan na Muungano wa upinzani wasaini rasmi azimio linaloashiria mwanzo wa utawala wa mpito wa Sudan

    (GMT+08:00) 2019-08-18 17:25:21

    Baraza la Mpito la Kijeshi la Sudan (TMC) na Muungano wa upinzani wa Uhuru na Mabadiliko jana walisaini rasmi azimio la kisiasa na kikatiba kuashiria mwanzo wa utawala wa mpito wa Sudan.

    Makamu Mwenyejkiti wa TMC Mohamed Hamdan Daqlu alisaini nyaraka mbili kwa niaba ya baraza la kijeshi, huku Kiongozi wa upinzani Ahmed Rabie akisaini kwa niaba ya Muungano wa upinzani. Baadhi ya maofisa waandamizi wa nchi na mashirika, wakiwemo mawaziri wakuu wa Misri na Ethiopia, walisaini nyaraka kama mashahidi. Akiongea baada ya hafla ya kutia saini mwakilishi wa Muungano wa upinzani wa Uhuru na Mabadiliko amewashukuru watu kwa kujitoa muhanga na kumwaga damu ili kuhakikisha siku hiyo inafika. Ameongeza kuwa kusainiwa kwa nyaraka kunaashiria awamu mpya, akiahidi kuwa kipaumbele cha kwanza kitakuwa ni amani kamili.

    Kwa upande wake mwenyekiti wa TMC Abdel-Fattah Al-Burhan amesisitiza vyombo vyote vya kijamii kushirikiana pamoja ili kufikia malengo ya mapinduzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako