• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali ya Hongkong yasema jambo muhimu kwa sasa ni kurejesha utaratibu wa jamii haraka iwezekanavyo

  (GMT+08:00) 2019-08-19 08:37:57

  Msemaji wa serikali ya mkoa maalumu wa Hongkong, China amesema jambo muhimu zaidi kwa sasa ni kurejesha utaratibu wa jamii haraka iwezekanavyo katika mkoa huo.

  Msemaji huyo amesema ingawa maandamano yaliyofanyika katika bustani ya Victoria yalikuwa ya amani, lakini kutokana na washiriki kuandamana katika barabara kuu kadhaa, usafiri wa umma uliathiriwa. Amesema idara ya uchukuzi na polisi wameshirikiana ili kupunguza athari hiyo kadri iwezekanavyo.

  Msemaji huyo amesisitiza kuwa, baada ya utulivu kurejeshwa, serikali ya Hongkong itafanya mazungumzo na raia, ili kujitahidi kuondoa mgawanyiko na kujenga upya masikilizano katika jamii.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako