• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Chelsea, Leicester, Man City na Spurs hakuna mbabe

  (GMT+08:00) 2019-08-19 10:46:11
  Ligi kuu ya Uingereza (EPL) imepigwa mwishoni mwa wikiendi hii kwa michezo mitatu, watoto wa daraja la Stamford Chelsea wametoka sare ya goli 1-1 dhidi ya Leicester City, huku Sheffield United ikiifumua Crystal Palace goli 1-0. Mchezo mwingine umepigwa baina ya Manchester City dhidi ya Tottenham Hotspurs, hadi kipenga cha mwisho cha mwamuzi wa mchezo, timu hizo zimetoka sare kwa kufungana mabao 2-2.

  Habari nyingine ni kuwa, kocha wa Man City Pep Guardiola amefafanua tukio lililotokea kati yake na mshambuliaji wake Sergio Aguero alipomtoa na kumuingiza Gabriel Jesus katika mechi dhidi ya Spurs.

  Pep amesema hana chuki na mchezaji yeyote, aliona anatakiwa kufanya mabadiliko na kuamua kumtoa Aguero na si vinginevyo ambavyo baadhi ya watu wameanza kutafsiri.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako