• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Yanga yafumua kikosi chake ikijiandaa mchezo wa maruadiano na Rollers ya Botswana

  (GMT+08:00) 2019-08-19 10:48:26
  Kocha wa klabu ya Yanga ya Tanzania raia wa DR Congo Mwinyi Zahera, amefumua kikosi chote cha klabu hiyo huku akisisitiza kwamba hafanyi mambo kwa ajili ya kufurahisha mashabiki. Zahera amesisitiza kuwa hata katika mechi ya kirafiki ya jana dhidi ya AFC Leopards ya Kenya hakuna mchezaji hata mmoja alliyecheza katika mechi ya kwanza ya kirafiki ambapo Yanga ilichapwa goli 2-0 na Polisi ya Moshi.

  Naye kaimu katibu mkuu wa klabu hiyo Dismas Ten amesema, Yanga itaondoka kesho kwenda Botswana kucheza mechi ya marudiano ya ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers huku ikiwakosa wachezaji wake watatu wa kimataifa ambao hawajapata leseni toka shirikisho la soka Afrika (CAF).

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako