• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kujenga mji wa Shenzhen kuwa eneo la kielelezo cha ujamaa wenye umaalum wa China

    (GMT+08:00) 2019-08-19 18:14:46

    Serikali ya China imetangaza kuunga mkono kuujenga mji wa Shenzhen kuwa eneo la kielelezo cha ujamaa wenye umaalum wa China, ili kusukuma mbele sera ya mageuzi na kufungua mlango, na kutekeleza vizuri zaidi mkakati wa eneo kubwa la ghuba ya Guangdong, Hong Kong na Macao.

    Mji wa Shenzhen ulioko kusini mwa mkoa wa Guangdong ni eneo maalumu la kwanza la kiuchumi nchini China kwa ajili ya majaribio ya sera ya mageuzi na kufungua mlango. Katika miaka 40 iliyopita, Shenzhen imeendelezwa kuwa jiji la kimataifa kutoka kijiji kidogo cha wavuvi kilichoko karibu na Hong Kong. Sasa mji huo umepata fursa tena ya kuwa eneo la kielelezo. Mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa uendeshaji wa miji ya China cha Chuo Kikuu cha Beijing profesa Li Guoping anasema,

    "Mji wa Shenzhen ni sehemu yenye mafanikio makubwa zaidi kutokana na sera ya mageuzi na kufungua mlango. Tukitaja sera hiyo ya China, tunakumbuka mji huo. Je, katika mchakato wetu wa kuijenga China iwe nchi ya kijamaa ya kisasa na yenye nguvu, mji wa Shenzhen unaweza kutoa uzoefu unaoweza kuigwa? Nafikiri hii ndio sababu ya kuuchagua kuwa eneo la kielelezo."

    Kufuatia waraka uliotolewa na serikali ya China, mji wa Shenzhen utakuwa "sehemu yenye maendeleo ya sifa ya juu", "mji wa kuigwa wa utawala wa kisheria", "mji wa kuigwa wenye ustaarabu mzuri", "vigezo vya maisha bora", na "mtangulizi wa maendeleo endelevu". Mji huo utajenga mfumo wa kisasa wa uchumi, mazingira wazi ya kibiashara na ya kiwango cha juu zaidi cha kimataifa, mfumo wa kiwango cha juu cha huduma za kijamii, mazingira mazuri ya kazi na maisha, na mazingira safi ya kiikolojia.

    Waraka huo pia umetoa ajenda ya maendeleo ya mji wa Shenzhen. Hadi kufikia mwaka 2025, mji huo utaongoza miji yote duniani kwa nguvu ya kiuchumi na sifa ya maendeleo, mwaka 2035, mji huo utashika nafasi ya kwanza duniani kwa nguvu ya kiuchumi, na mwaka 2050, utakuwa mji wenye nguvu kubwa zaidi za ushindani, uvumbuzi, na ushawishi. Mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa utalii na nyumba cha taasisi ya utafiti wa mambo ya uendelezaji ya China Bw. Song Ding anasema,

    "Tuna majukumu ya kufungua mlango zaidi, na hata nchi yetu ina majukumu ya kuongoza maendeleo ya dunia katika siku za baadaye. Hivyo ni lazima tujenge eneo hilo la kielelezo, ambalo ni tofauti na eneo maalum la kiuchumi."

    Katika waraka huo, serikali ya China pia imetaka mji wa Shenzhen kuharakisha kuanzisha hali mpya ya kukuza mageuzi na kufungua mlango, kufanya majaribio ya mageuzo ya kampuni zinazomilikiwa na serikali, kujenga maeneo ya majaribio ya biashara huria, na kuhimiza ujenzi wa eneo kubwa la ghuba la Guangdong, Hong Kong na Macao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako