• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afisa wa ngazi wa juu wa Hong Kong asema hali ya hivi karibuni ni ya hatari zaidi kushuhudiwa katika miaka 25

    (GMT+08:00) 2019-08-19 19:01:13

    Wakati maandamano yenye vurugu yakiingia mwezi wa tatu sasa huko Hong Kong, Supritendedi Mkuu wa polisi ya Hong Kong ambaye ni Muingereza David Joardan amesema kwenye mahojiano kuwa hali ya sasa ni ya hatari zaidi kuwahi kuikabili katika miaka 25 iliyopita, na waandamanaji wanaonekana kujipanga vizuri na wako tayari kwenda zaidi ya hapo ili kutimiza ajenda yao husika.

    Jordan mwenye miaka 52 ambaye amejiunga na polisi ya Hong Kong mwaka 1992, anatumikia kama Kamanda wa kikosi cha Ufundi cha Polisi, ambacho kinashughulikia hali ya dharura. Amesema kitu kinachoonekana ni kuwa waandamanaji wako tayari kuzidi kutumia njia ya vurugu na uharibifu ili kuleta machafuko, na kusisitiza kuwa anaamini kama watapata nafasi ya kuwajeruhi au kuwaumiza polisi, basi watafanya hivyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako