• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa kwanza wa baraza la bustani la taifa wafunguliwa

    (GMT+08:00) 2019-08-19 20:55:27

    Rais Xi Jinping wa China ametoa barua akipongeza kufunguliwa kwa mkutano wa kwanza wa baraza la bustani la taifa na kuwakaribisha wageni kutoka nchi mbalimbali na watu kutoka jamii mbalimbali wanaohudhuria mkutano huo.

    Kwenye barua hiyo rais Xi amesema, ujenzi wa ustaarabu wa kiikolojia una maana kubwa kwa maendeleo ya ustaarabu wa binadamu. Miaka ya hivi karibuni, China imeshikilia msimamo ambao maji safi na milima inayostawi ni mali kubwa, kushikilia usimamizi wa mifumo wa milima, maji, misitu, mashamba, maziwa na mbuga, na kutekeleza mfumo wa bustani za taifa.

    Amesisitiza kuwa China kuimarisha ujenzi wa ustaarabu wa kiikolojia sio tu kunalingana na hali ya China, bali pia ni kujifunza uzoefu wa mafanikio ya nchi za nje. Mbali na hayo rais Xi ametoa wito kwa mkutano huo wenye kaulimbiu ya "Kujenga mfumo wa hifadhi ya kimaubile yenye kiini cha bustani ya taifa" kufanya majadiliano ya kina na kukusanya mashauri na mapendekezo, ili kushirikiana kutoa mchango katika ujenzi wa siku nzuri zaidi za mbele za ustaarabu wa kiikolojia wa dunia na kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako