• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • mechi za marudiano ligi ya mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho kupigwa wikiendi hii

  (GMT+08:00) 2019-08-20 08:17:30
  Wawakilishi wa Tanzania katika mechi za kimataifa msimu huu, Simba, Yanga, KMC na Azam za Tanzania na Malindi na KMKM za Zanzibar zinavibarua vigumu vya kuhakikisha zinashinda mechi za marudiano ya ligi ya mabingwa na Kombe la Shirikisho barani Afrika ili zisonge mbele kwenye michuano hiyo.

  Simba, Azam na KMC zitakuwa viwanja vya nyumbani wakati Yanga, Malindi na KMKM zitakuwa ugenini. Simba itarudiana na UD Songo ya Msumbiji katika ligi ya mabingwa huku KMC itaumana na AS Kigali kwenye kombe la shirikisho.

  Yanga wao wamewafuata Township Rollers ya Botswana, nayo Azam watakutana na Fasil Kenema ya Ethiopia. KMKM itarudiana na Agosto ya Angola na Malindi watavaana na Mogadishu City ya Somalia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako