• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya yawapiku vigogo viwango vya dunia

  (GMT+08:00) 2019-08-20 08:17:49
  Timu ya taifa ya raga ya Kenya Lionesses imeingia katika 25 bora kwenye viwango bora duniani vya mchezo wa raga ya wanawake ya wachezaji 15 kila upande vilivyotangazwa jana.

  Kenya imeipita Denmark, Fiji na Jamaica baada ya kushirikia michuano ya kombe la dunia jijini Johannesburg Afrika Kusini ilikoilipua Madagascar kwa miguso 35-5 na Uganda 37-5 kabla ya kuzidiwa ujanja na wenyeji Afrika Kusini kwa miguso 39-0 kwenye fainali iliyopigwa mwishoni mwa wikiendi.

  Vimwana hao wanaofundishwa na kocha Oloo, ambao sasa watalazimika kushinda mchujo wa dunia utakaoleta pamoja timu kutoka Amerika Kusini, Ulaya, Asia na Oceania mwaka 2020 ili kuingia Kombe la dunia mwaka 2021 nchini New Zealand, wameimarisha alama zao kutoka 46.46 hadi 46.72 kwenye viwango hivyo vya mataifa 55.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako