• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Guardiola apagawa na VAR, adai inapendelea

    (GMT+08:00) 2019-08-20 08:18:44
    Kama kuna jambo linalomchanganya sasa Pep Guardiola kocha wa Manchester City ni mfumo wa teknolojia ya video ya kutambua goli (VAR) kwa kudai kuwa inachagua matukio na anaamini inatumika vibaya.

    Pep kwa mara nyingine alishuhudia VAR ikiinyima ushindi timu yake dhidi ya Tottenham baada ya bao la Gabriel Jesus kukataliwa katika dakika za majeruhi.

    Kocha huyo ametoa mfano wa mpira ulioguswa na mkono na beki wa Chelsea, Andreas Christensen kwenye mchezo wa Super Cup dhidi ya Liverpool wiki iliyopita lakini mwamuzi hakutoa penalti. Amesema inabidi warekebishe kwani matukio ndani ya uwanja hayako wazi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako