• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi Jinping atoa wito wa kuhifadhi kiini halisi cha utamaduni wa China

  (GMT+08:00) 2019-08-20 20:20:43

  Katibu mkuu wa kamati kuu ya Chama cha Kikomusiti cha China, Xi Jinping ametoa wito wa kuhifadhi kiini halisi cha utamaduni wa China.

  Rais Xi ametoa wito huo jana kwenye kongamano lililofanyika kwenye Akademia ya Dunhuang akiwa pamoja na wataalamu, wasomi na wawakilishi husika kutoka vitengo vya utamaduni, wakati akifanya ziara ya ukaguzi mkoani Gansu, China.

  Aidha rais Xi amesisitiza haja ya kusaidia kuendeleza na kuhimiza utamduni wa jadi. Pia ametaka kufanywa juhudi zaidi katika kubadilishana utamaduni na nchi nyingine na kujifunza kutokana na mafanikio makubwa ya ustaarabu duniani kote. Katika ziara yake ya ukaguzi rais Xi alitembelea Mapango ya Mogao huko Dunhuang eneo muhimu la urithi wa utamaduni ambalo linalindwa kitaifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako